Pakistan imegundua wagonjwa watatu na virusi vya mpox, idara ya afya katika mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa ilisema.
Idara hiyo mnamo Ijumaa ilisema kwamba maambukizi ya virusi yaligunduliwa kwa wagonjwa walipofika kutoka Falme za Kiarabu.
Wizara ya afya ya Pakistani imesema siku ya Ijumaa kwamba haikugundua aina yoyote mpya ya pox nchini humo, shirika la habari la Reuters liliripoti.
Shirika la Afya Duniani limetangaza mlipuko wa hivi majuzi wa ugonjwa huo kama dharura ya afya ya umma ya wasiwasi wa kimataifa baada ya aina mpya ya virusi kutambuliwa.