Pambano la uzito wa juu la bondia Anthony Joshua dhidi ya Kubrat Pulev limelazimika kuahirishwa kwa muda usiojulikana kutokana na janga la virusi vya corona lililoathiri mambo mbalimbali.
Pambano hilo awali lilikuwa limepangwa kuchezwa June 20 katika uwanja wa Tottenham Hotspurs jijini London England lakini licha ya kuwa mbali corona imeathiri vitu vingi katika pambano hilo ikiwemo maandalizi.
Bado haijathibitika kwa asilimia 100 kama pambano hilo litachezwa lini lakini kwa mujibu wa promota wa Anthony Joshua anayejulikana kwa jina la Eddie Hearn anatazamia pambano hilo lichezwe July 25 pale pale Tottenham kama maambukizi ya virusi vya corona yatakuwa yamemalizika au wataalam wakithibitisha kuwa wanaweza kuendelea.