Mtu wangu wa nguvu nadhani utakua umeipata taarifa ya ugunduzi wa dawa ya uzazi wa mpango wa panya, vilevile utakua umesikia lakini unaweza ukawa haujaipata vizuri kiundani habari hii, Ayo TV imempata mgunduzi wa dawa hiyo Ginethon Mhamphi kutoka kituo cha utafiti na udhibiti viumbe waharibifu kutoka Chuo cha SUA Morogoro.
Mgunduzi huyo amesema…….>>>’hii ni njia ya kibaolojia na ni njia ambayo gharama yake ni nafuu ikilinganishwa na matumizi ya sumu, hii ni njia ya kiubindadamu kwa sababu huyu mnyama hafi, hateseki hatakuwa anabaki tu kwenye mazingira yake isipokuwa hataweza kuzaa kwa muda ambao tutataka asizaliane’
Utafiti huo kwa Afrika ndio wa kwanza kufanyika na kingine ni kuhusu dawa hii ni kuwa inaweza kufanya kazi kwa binadamu na haina madhara yoyote…………>>’hii dawa ni ileile ambayo inayoweza kufanya kazi kwa binadamu ila kwa form tofauti ya vidonge ambazo wa kina mama huwa wanameza;-Ginethon Mfawidhi
Unaweza kutazama video hii hapa chini
ULIKOSA HII YA JAMAA ALIVYOIGIZA SAUTI ZA LOWASSA, ANNE MAKINDA NA MBOWE? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI