Kiungo mkabaji wa zamani wa timu ya taifa ya Senegal Papa Bouba Diop ,42, amefariki dunia leo Paris nchini Ufaransa baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Diop bado vyanzo vingi vya habari havijaweka wazi sababu za kifo chake lakini inaripotiwa alikuwa akiugia kwa muda mrefu.
Papa Diop umaarufu mkubwa aliupata 2002 katika fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Korea na Japan baada ya kufunga goli na kuipa ushindi 1-0 wa Senegal dhidi ya Ufaransa ambao ndio walikuwa Mabingwa watetezi lakini walifika pia hatua ya robo fainali katika michuano hiyo huku Diop akifunga magoli mawili katika sare ya 3-3 dhidi ya Uruguay.
Papa Diop amewahi kucheza vilabu mbalimbali England kama Fulham, Portsmouth, West Ham United na Birmingham City, Diop alistaafu timu ya taifa 2008 na soka kwa ujumla alistaafu 2013.