Papa Francis siku ya Jumatano alishutumu sekta ya silaha kwa “kunufaika na vifo vinavyo tokea katika sehemu mbalimbali duniani.”
Akihutubia umati wa watu huko Vatikani kwa Hadhira yake Kuu ya Jumatano, papa alisema, “Leo uwekezaji ambao hutoa mapato mengi ni viwanda vya silaha.”
“Kufaidika kutokana na kifo ni mbaya,” aliongeza, kulingana na Vatican News.
Akiwataka Wakatoliki wasisahau kuombea amani na wahanga wa vita, alikariri: “Vita ni kushindwa siku zote.”
Kisha akatoa wito wa maombi hasa kwa wale wanaoteseka kutokana na vita vinavyoendelea nchini Ukraine na Palestina.
Francis pia aliangazia hali mbaya ya wakimbizi wa Rohingya nchini Myanmar, ambayo inakabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
“Tuombe amani, tuombe amani ya kweli kwa watu hawa na dunia nzima,” aliongeza.