Papa Francis amewasili Timor Mashariki, taifa dogo lenye idadi kubwa ya Wakatoliki nje ya Vatican, akiwa kwenye ziara yake ya Asia na Pasifiki.
Maelfu ya raia wa Timor walijipanga mitaani kumpokea kwa shangwe, hata hivyo, Ziara ya Papa pia inaweka uchunguzi mpya juu ya Janga la unyanyasaji wa kijinsia katika Kanisa,
Miaka miwili iliyopita, Vatikani ilikiri kwamba ilimwadhibu kwa siri Askofu wa Timor Mashariki na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Carlos Ximenes Belo, baada ya kushutumiwa kwa kuwanyanyasa Wavulana kingono miongo kadhaa.
Pia, kuna shauku kubwa ikiwa Papa Francis atashughulikia moja kwa moja suala hilo akiwa Timor Mashariki, kama anavyofanya katika safari zilizopita nje ya nchi, ingawa hatua hiyo haipo kwenye mpango rasmi wa ziara yake.
Baadhi ya wachambuzi wamesema iwapo Papa Francis atashughulikia dhuluma hiyo akiwa Timor Mashariki, huenda ingetuma ujumbe mzito kwa walionusurika na wale ambao hawajajitokeza, iwe Nchini au karibu na eneo hilo.
Aidha Timor Mashariki, ikiwa na asilimia 97 ya Wakatoliki, ni Nchi ya pili yenye Wakatoliki wengi zaidi Duniani, Serikali ya Timor imetenga Dola milioni 12 kwa ajili ya Ziara hii, kiasi ambacho kimekosolewa kutokana na hali ya kiuchumi ya Taifa hilo maskini.