MWANANCHI
Mahakama Kuu Dar es Salaam imewahukumu kunyongwa washtakiwa sita, Mashaka Pastory, John Mndasha, Martime Mndasha, Haji Kiweru, Wycliff Imbora na Rashid Abdikadir baada ya kukutwa na hatia ya kupora pesa milioni 150/- za Benki ya NMB na mauaji ya Askari wa FFU na mfanyakazi mmoja wa Benki hiyo.
Jumla ya vielelezo 78 vya ushahidi viliwasilishwa Mahakamani mbele ya Jaji Projest Rugazia kwenye kesi hiyo na kubaini washtakiwa hao walikuwa na hatia.
Washtakiwa hao walitenda kosa hilo siku ya tarehe 20, 2006 ambapo uporaji wa fedha hizo pamoja na tukio la mauaji lilifanywa na washtakiwa hao wakati walipokuwa wakisafirisha fedha hizo kutoka Dar kwenda Morogoro.
MWANANCHI
Hospitali ya CCBRT na Chama cha Wamiliki wa Mabasi yaendayo Mikoani (TABOA) wamezindua kampeni ya kitaifa dhidi ya Fistula ya uzazi ambayo lengo lake ni kusambaza taarifa kuhusiana na ugonjwa huo na upatikanaji wa tiba yake.
Tangu kuzinduliwa kwa kampeni ya ugonjwa huo wanawake zaidi ya 1,308 wamepata tiba ya ugonjwa huo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mganga Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Magreth Mhando amesema kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha mgonjwa wa Fistula inatibika.
NIPASHE
Watoto watatu Rafael Bruno, Meshack Gasper na Juvens Bathoromeo wamefariki kutokana na kuungua kwa moto ambao waliuwasha kwa lengo la kuwinda wanyama katika msitu Kilosa, Morogoro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo anasema moto uliwazunguka watoto hao na kushindwa kupata mahali pa kutokea, mpaka wakakutwa na umauti eneo hilo.
MTANZANIA
Kauli ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka aliyoitoa juzi kwa vyombo vya habari kwamba yeye na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Muhongo hawatojiuzulu kwa kuwa Rais Kikwete anawategemea imeonekana kuwatibua wasomi, wanasiasa na watu wa kada mbalimbali.
Baadhi yao ikiwemo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu CUF, Julius Mtatiro aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Facebook uliosomeka hivi; “Hata kama ulifeli magazijuto huwezi kujua fomula hii, kwa wanaojua maana ya ‘pre-emption’ watakubaliana nami kwamba taarifa ya Ikulu juu ya Mwanasheria Mkuu kuachia ngazi iliyokuwa imejaa bashasha na sifa kuu kwake ilikuwa na maana ya kuanza safari ya kulinda wezi wa fedha za umma.”
Mhadhiri na Mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana amesema; “Nafikiri Profesa anatakiwa kusoma alama za nyakati, anatakiwa kuona kwamba jamii tayari imekwishahukumu, lakini pia anatakiwa kufahamu kuwa wakati mwingine kama mwanasiasa unapaswa kuwajibika kwa ajili ya kujenga heshima yako”
Bunge lilitoa maazimio ya kutaka watu wanaohusishwa na uchotaji wa pesa za umma zaidi ya bili. 300 kwenye akaunti ya Escrow kuwajibishwa ambapo mpaka sasa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema amejiuzulu.
HABARI LEO
Mabasi 11 ya abiria Lindi yamekamatwa na SUMATRA kwa kutuhumiwa kupandisha nauli kutoka 22,000/- mpaka 35,000/- kwa abiria mmoja kutoka Lindi kwenda Dar es Salaam.
Msimamizi wa SUMATRA Lindi, David Nyanda amesema mabasi hayo yalipigwa faini y ash. 250,000/- kila moja huku akiyataja mabasi hayo kuwa ni Mwana wa Mwanza na Machinga Bus.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook