Martha Nagbe alijikuta akitozwa faini na Mahakama kwa kesi ya usumbufu na kupigia kelele majirani na wapita njia, lakini ukweli ni kwamba alipigwa faini hiyo kutokana na kufanya mahubiri barabarani kwa sauti ya juu na sio kwamba alikuwa akipiga kelele.
Mke huyo wa mchungaji ambaye amekutana na mkasa huo Dakota, Marekani amepigwa faini hiyo baada ya kukutwa mara kadhaa akihubiri barabarani jirani na makazi ya watu ambao nao waliwahi kulalamika kwamba wanakerwa na kelele za mama huyo, mwisho wa siku Polisi wa doria walimkuta na kumpeleka Mahakamani ambako alipigwa faini ya dola 150 ambazo ni zaidi ya 270,000/- Tshs.
Mume wa mwanamke huyo Mchungaji Juwle Nagbe amesema mke wake amesikitishwa sana na maamuzi ya Mahakama hiyo na anauona kama ni uonevu.
Mbali na kupigwa faini hiyo Martha amesema hatoacha kusali kwa sababu ana imani na MUNGU na pia anaamini yuko huru kuendelea kufanya mahubiri kwa njia yoyote ambayo ataona iko sawa na imani yake.
Kwa huku kwetu tumezoea kuwaona watumishi wakihubiri maeneo mbalimbali ya mikusanyiko ya watu kama stendi za daladala, sokoni lakini kumbe kwa wenzetu ni ishu kama ukikamatwa.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook