Kiongozi wa dhehebu nchini Kenya ambapo mamia ya watu wanaodaiwa kufariki kutokana na njaa ameshtakiwa kwa makosa 191 ya mauaji.
Paul Mackenzie na wenzake 29 walikana mashtaka mbele ya mahakama moja katika mji wa pwani wa Malindi.
Zaidi ya miili 400, ikiwa ni pamoja na ile ya watoto, ilifukuliwa kutoka makaburi ya kina kirefu kwenye kipande cha ardhi kinachodhaniwa kuwa kinamilikiwa na mhubiri huyo mwenye utata.
Awali alishtakiwa kwa vitendo vya kigaidi, ukatili wa watoto na mateso, mashtaka ambayo aliyakanusha. Tayari anatumikia kifungo cha mwakammoja kwa kutengeneza na kusambaza filamu zenye mahubiri yake yenye utata – bila leseni.
Waathiriwa kulingana na BBC waliambiwa kufunga mpaka waende mbinguni. Paul Mackenzie aliwahi kusema kuwa hakumlazimisha mtu yeyote kufunga.