July 01 2015 tayari imefika, kumekucha na stori nyingine nyingi Magazetini, hizi ni sehemu ya stori kubwa zilizotawala leo.
Wafanyabiashara walioficha mafuta walalamikiwa, Wabunge watapata mafao yao ya Mil. 230 kila mmoja mwezi huu baada ya Rais JK kuvunja Bunge.. Rais Ali Mohammed Shein amewataka Wanasiasa kuacha kuivuruga Z’bar wakitumia mfumo wa Serikali ya umoja ya Kitaifa.
Stori nyingine inahusu Waziri Membe kutoa ufafanuzi kuhusu Mabilioni ya Libya, TAKUKURU imesema wananchi wawapime Wanasiasa wanaotumia Fedha kutaka wachaguliwe..
Membe amesema hatamuunga mkono Mgombea yoyote atakayeteuliwa na CCM, Mbunge wa Igunga na Naibu Waziri wa Nishati na Madini almanusura wapigane baada ya kutokea majibizano, Zitto Kabwe ameahidi kuyataja majina ya Watanzana 99 walioficha Mabilioni ya Uswisi.
Mengine ni kutoka Bagamoyo, taharuki imeibuka baada ya mwili wa marehemu kutokwa jasho na kutikisika kabla ya kuzikwa, TBS imeteketeza mabati zaidi ya 2,000 yaliyoagizwa toka India… NEC imelaumiwa kucheleweshwa Kuandikisha Wapigakura kwenye BVR.
Iko sauti ya Rais JK akizungumzia kuhusu ishu ya Changamoto zilizojitokeza mashine za BVR.. Kama ulipitwa na PowerBreakfast unaweza kuisikiliza hapa.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.