Kingine ambacho nimeona nikusogezee leo MAY 21 2015 ni huu uchambuzi wa Stori za Magazetini.
Stori kubwa ni kuhusu siku ya leo ambayo ni kumbukumbu ya ajali ya meli ya MV Bukoba ambayo ilipata ajali mwaka 1996.. Kwenye zilizochambuliwa iko pia stori ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU amesema uchunguzi unaanza kwa wahusika wa ubadhilifu wa fedha za umma kutokana na Ripoti ya CAG, Mwigulu Nchemba amesema Serikali imeshatoa fedha za wanafunzi wa Vyuo Vikuu TZ.
Ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu imesema Jeshi la Polisi lilitumia nguvu kuwakamata viongozi wa CUF na wanachama wake Mbagala, watu wa Dar wako hatarini kupata magonjwa mbalimbali kutokana na nyama inayochinjwa kutopimwa.
Hospitali ya Rufaa Mbeya imepiga marufuku ‘wanaovaa ovyo’ kuingia Hospitali hiyo, Mbunge wa Rombo amewajia juu Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro ameunda Tume kuchunguza sakata la Mtumishi aliyesimamishwa kazi KCMC kwa kumtumia message Rais JK, nyingine inatokea Rombo ambapo Mbunge wa Jimbo hilo amemjia juu Mkuu wa Wilaya kujiuzulu kutokana na kushindwa kuwajibika baada ya kuandiikwa stori kwamba wanawake wa Rombo wanakodi wanaume toka Kenya ili wafanye nao tendo la ndoa.
Unaweza kuzisikia hizo na nyingine zote kwa kubonyeza play hapa, hii nimeirekodi #PowerBreakfast @CloudsFM
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.