May 23 2016 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu alizindua huduma ya longa nasi kata mnyororo wa rushwa ambayo imeanzishwa na Taasisi ya kupambana na Rushwa Tanzania Takukuru.
Huduma hiyo inawawezesha wananchi kupiga simu na kutoa taarifa za Rushwa kwa kupiga namba 113 au *113# yote ni kusaidia wananchi badala ya kwenda ofisi za Takukuru watakuwa wanatoa taarifa ambazo zitazingatia usiri.
Leo May 26 2016 imetolewa taarifa na kaimu mkuu wa idara ya uratibu na utoaji habari elimu kwa Umma, Matai Kirumbi kwamba wamepokea zaidi ya taarifa 8000 mpaka jana May 25 ambapo wameanza kuzifanyia kazi.
ULIIKOSA HII YA ZITTO KWANINI TAKUKURU HAWAJAWAFIKISHA HAWA MAHAKAMANI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE