Nchi ya Nigeria, jana April 13, 2018 ilikuwa ikiadhimisha kitaifa miaka 4 tangu kutendeka tukio la utekwaji wa watoto wakike zaidi ya 200 katika shule ya Government Girls Secondary School mjini Chibok.
Rais wa nchi hiyo Muhammadu Buhari katika maadhimisho hayo amewahakikishia wazazi wa wasichana hao waliotekwa na bado hawajaachiliwa huru kuwa serikali yake inafanya iwezalo kuwaokoa mabinti hao.
Aliwaomba wazazi kuendelea kuwa na tumaini kwamba wasichana hao 112 ambao wanashikiliwa mateka na magaidi hao wa kikundi cha Boko Haram wataokolewa kipindi ambacho masharti yaliyotolewa na watekaji yatakaa sawa.
Binti mwenye ugonjwa wa kutonenepa