Leo April 18, 2018 Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limeeleza kuwa watoto wanajeshi zaidi ya 200 wameachiliwa huru huko Sudan Kusini.
Jumla ya watoto wa kiume 112 na wakike 95 ambao wengine walikuwa na chini ya umri wa miaka 14 waliachiliwa huru katika sherehe maalumu ya ‘kuweka chini silaha’ iliyoandaliwa na UNICEF jana katika mji wa Yambio.
Shirika hilo la UN limeeleza kuwa linatumaini kuachiliwa watoto 1000 zaidi katika miezi ijayo na kwamba tayari watoto zaidi ya 500 tayari wamekwisha achiliwa huru mwaka huu 2017.
Maelfu ya watoto wamelazimishwa kujiunga na vikosi vya kijeshi na vikundi vingine vya silaha nchini Sudan Kusini tangu nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta ilipokua na vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013.
Takribani watoto 19,000 wanafanya kazi katika vikosi vya silaha na vikundi mbalimbali nchini humo, hii ni kulingana na takwimu zilizotolewa na shirika hilo.
Maagizo ya Naibu Waziri Shonza Bungeni leo