Kampuni za migahawa ya McDonalds imetangaza kuwa hivi karibuni itaondoa kabisa mirija ya plastiki inayotumika hivi sasa katika migahawa yake yote ya nchini Uingereza.
Kampuni hiyo imeeleza kuwa tayari vifungashio vyote, vya chakula kinachotengenezwa na migahawa hiyo vinaweza kutengenezwa tena yaani ‘recycled‘ lakini mirija hiyo imeshindikana.
Kutokana na hili migahawa hiyo imepanga kuanza kutumia mirija iliyotengenezwa kwa makaratasi na mirija hiyo itaanza kutumika mwezi May, 2018 katika migahawa yake 1,300 nchini Uingereza.
UFAFANUZI: Tanzania, Kenya hatiani kupasuka vipande viwili kujitenga na Afrika