Baada ya aliyekuwa nyota wa timu ya Taifa ya Brazil Edson Arantes do Nascimento maarufu kama Pele kuugua kwa muda wa miezi sita, hatimaye uongozi wa hospitali ya Sao Paulo, Brazil imefikia maamuzi ili kuokoa maisha yake.
Wataalam wameamua kumfanyia Pele upasuaji wa kibofu cha mkojo katika hospitali hiyo ili kuondoa mawe yaliyokuwa yakimsumbua katika figo yake
Pele mwenye umri wa miaka 74 alilazwa katika hospitali hiyo takriban miezi sita.
Pele ambaye jina lake ni Edson Arantes do Nascimento alifunga zaidi ya mabao 1200 wakati alipokuwa akicheza soka na kuisaidia Brazil kushinda mataji matatu ya kombe la dunia.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.