Kuna hii ya kuifahamu leo September 9, 2020 kutoka Kenya ambapo Everlyne Njoki (22) ambaye alipigwa risasi mara 6 wiki mbili zilizopita amemsamehe Mpenzi wake ambaye pia ni Polisi baada ya kutoka Hospitali.
Baada ya kurejea nyumbani Everlyne amesema hana kinyongo na David Nyamweya na jambo la muhimu ni uhai, hivyo anataka kuendelea na maisha yake.
“Nilipigwa risasi na Mpenzi wangu ambaye ni Polisi lakini nimemsamehe kutokana na upendo MUNGU alionao kwangu, amenisaidia na ameokoa maisha yangu, nipo hai kwa sababu ya neema zake, hivi sasa nataka kumtumikia”Everlyne
Polisi wamesema baada ya msako mkali Mtuhumiwa amekamatwa na atafunguliwa mashataka ya kujaribu kujaribu kumuua Everlyne.