Mama mzazi wa kocha wa Man City Pep Guardiola anayejulikana kwa jina la Dolors Sala Carrio ,82, amefariki dunia kwa maambukizi ya virusi vya corona jijini Barcelona Hispania.
Hispania ni miongoni mwa nchi za Ulaya zilizoathirika kwa kiwango kikubwa, kiasi cha raia wake kuamuliwa kukaa nyumbani kama sehemu ya kupunguza maambukizi.
Pep Guardiola ni miongoni mwa watu waliojitoa kupambana katika vita dhidi ya virusi vya corona, kiasi cha kufikia maamuzi ya kutoa msaada wa euro milioni 1 (Tsh Bilioni 2.4) kwa taasisi ya Angel Soler Daniel Foundation na Medical College kwa ajili ya kununua vifaa vya mapambano dhidi ya corona.