Kocha wa klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani ambaye mwishoni mwa msimu huu atakuwa kocha wa klabu ya Man City ya Uingereza Pep Guardiola, February karudi tena kwenye headlines baada ya kutoa kauli ya kuchekesha kidogo wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Pep Guardiola February 5 ameingia kwenye headlines ikiwa ni siku chache zimepita toka atangaze kuwa mwishoni mwa msimu atakuwa kocha wa klabu ya Man City, hivyo yupo FC Bayern Munich kumalizia msimu huu, swali likaja kwa Guardiola kuwa haoni kuwa ataathiri timu yake ya FC Bayern Munich baada ya kuthibitika kuwa ataondoka FC Bayern na kujiunga na Man City?
“Kama nilivyowaeleza naenda Uingereza kitu ambacho mnatakiwa kuaniamini, kuhusu kunpunguza umakini ndani ya FC Bayern Munich kwa sababu nitahama mwisho wa msimu, hapana mimi kama mwanamke naweza kufanya vitu vingi kwa umakini na kwa wakati mmoja, naweza kumudu na kufikiria vitu vyote” >>> Pep Guardiola
https://youtu.be/fU1jH7KYJLE
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.