Ukizungumzia headlines za usajili wa soka barani Ulaya kwa vilabu na wachezaji bado wamekuwa wakihusishwa kwenda katika vilabu mbalimbali na wengine kuongeza mikataba, ila ishu ipo kwa kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast anayeichezea Man City Yaya Toure kuwa hataenda klabu gani baada ya Guardiola kuonesha kutomuhitaji.
Tayari wakala wa Yaya Toure ameshathibitisha kuwa kiungo huyo ataondoka Man City mwezi January, hiyo inatokana na kutoorodheshwa na Guardiola katika kikosi cha wachezaji 21 watakaocheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2016/2017.
Headlines zilizoandikwa na Sky Sports kwa sasa ni kuwa Man United na Arsenal wameonesha nia ya kumuhitaji Toure na tayari walikuwa wamehusishwa kuzungumza na wakala wake kabla ya muda mchache kusema kuwa uhamisho wa nyota huyo kujiunga na vilabu hivyo bado ni mgumu.
Toure’s agent has claimed he has been subject to interest from #MUFC and #AFC as he looks to leave the Etihad #SSNHQ https://t.co/2aDFAFqrdM
— Sky Sports News HQ (@SkySportsNewsHQ) September 6, 2016
GOAL AND HIGHLIGHTS: YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1