Klabu ya Manchester United imekuwa ikimuwania beki wa Real Madrid ya Hispania Sergio Ramos kwa muda mrefu licha ya kuwa Real Madrid walikataa kumuuza beki huyo kwenda Manchester United kwani bado walikuwa wanahitaji huduma yake. Man United walikuwa na matumaini ya kumsajili Ramos baada ya yeye kukiri kutokuwa na furaha Real Madrid.
Baada ya Rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez kutangaza kuwa wamefikia makubaliano ya kuongeza mkataba na Ramos, Man United wamebadili mawazo yao na kukubali yaishe ila wamegeuzia mawazo na akili zao kwa beki wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid.
Man United wamegeuzia mawazo yao kwa Képler Laveran Lima Ferreira Pepe ambae amebakiza mkataba wa mwaka mmoja Santiago Bernabeu, Man United bado wanaonyesha dhamira ya kweli ya kutafuta beki mwenye kiwango cha juu licha ya kuwa bado Madrid wanamuhitaji aongeze mkataba.
Hata hivyo Man United bado wamesimamia msimamo wao wakutaka Pepe ahusishwe kwenye uhamisho wa golikipa wa Man United David De Gea kwenda Real Madrid kama ilivyokuwa kwa Ramos. Madrid wanafahamika kwa utamaduni wao wakutopenda kumuachia mchezaji wanayempenda kirahisi kwani Pepe yupo na klabu hiyo toka mwaka 2007 akitokea FC Porto ya Ureno.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos