Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Njombe Wilferdy Willa ameitaka Jami Mkoani humo hususani Wanaume kutambua kuwa fedha inavotafutwa na Mwanamke aliye kwenye ndoa ni ya kwake binafsi lakini fedha inavotafutwa na Mwanaume ni va Familia jambo ambalo litasaidia kutatua migogoro ya ndoa.
Ameongeza kuwa wanaume wengi kwenye ndoa hudhani pesa inayotafutwa na Mwanamke ndani ya ndoa ni ya Familia (wote) jambo ambalo sio sahihi kwa mujibu wa sheria ya ndoa badala yake Mwanamke ana wajibu wa kuwajibika kupitia fedha yake endapo tu Baba hayupo, amefariki au hawezi kutekeleza majukumu kwa wakati huo.
“Mwanaume au Mwanamke ukijua majukumu yako kwenye
Familia hakutakuwa na kelele, ukisoma sheria ya ndoa inasema Baba atawajibika kuhakikisha Familia yake inakuwa na ustawi na Mwanamke atafanya majukumu ya Baba kama Baba hayupo au hana uwezo wa kutekeleza majukumu kwa wakati huo, kwahiyo fedha inayotafutwa na Mwananke ni ya kwake na inayotafutwa a Mwanaume ni ya Familia”
AyoTV imezungumza na mwanasheria ambaye amefafanua Kwa Urefu zaidi kuhusu Sheria ya Ndoa inavyoeleza juu ya Pesa na mali za wanandoa, Pamoja na Mwijaku aliyetoa ufafanuzi kuhusu anavyoishi na mwanamke wake.
Play hapa chini kusikiliza:
PESA YA MKE, MUME HAIKUHUSU, SHERIA IMESISITIZA MWIJAKU APINDUA “NAPEWA HELA NA MKE WANGU”