Mwanamuziki Peter Morgan (46)maarufu kama Peetah, ambaye ni kiongozi wa kundi la Morgan Heritage nchini Jamaica amefariki dunia jana Februari 25.
Taarifa ya kifo chake imetolewa kwenye ukurasa rasmi wa Instagram wa kundi hilo, lakini haijaweka wazi sababu ya kifo chake.
Kundi la Morgan Heritage liliundwa mwaka 1994, likiongozwa na Peetah huku likijumuisha ndugu watano, watoto wa msanii wa reggae Denroy Morgan akiwamo Una Morgan, Roy ‘Gramps’ Morgan, Nakhamyah ‘Lukes’ Morgan na Memmalatel ‘Mr Mojo’ Morgan.
Peetah akiwa kwenye kundi hilo alifanikiwa kushirikiana na wasanii mbalimbali wa Tanzania akiwamo Diamond Platnumz kwenye wimbo wake wa ‘Hallelujah’, Harmonize wimbo ‘Malaika’ na Romy Jons wimbo ‘Ready.’