Mwanamke mmoja amejiua baada ya kuua watoto wake wawili, mmoja wa miaka sita na mwingine wa miaka minne katika kijiji cha Vumilia huko jijini Nairobi nchini Kenya.
Inaelezwa kuwa mwanamke huyo alifanya tukio hilo kwa madai ya mume wake kuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa. Mwanamke huyo pamoja na watoto wake wanaelezwa kunywa sumu kabla ya mama huyo kuwanyonga watoto hao na yeye mwenyewe kujinyonga.
Mwanamke huyo ambaye jina lake halijatajwa kabla ya tukio hilo aliandika ujumbe kwaajili ya mumewe kuwa sasa anaweza kufurahia uhuru wake wa kuwa na uhusiano na mwanamke wake huyo aliyemtaja kwa jina la Mueni.
BREAKING: CHADEMA wanaongea na Waandishi wa Habari