Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Paramagamba Kabudi amelieleza Bunge kuwa wamefanya mazungumzo na kampuni ya madini ya Tanzanite One ambapo amesema kampuni hiyo wamekiri makosa waliofanya hivyo watalipa kodi na tozo zote na watatoa fidia kwa Serikali na mpaka sasa fidia ya awali wameshalipa lakini hawatataja.
‘Tunaishi dunia ambayo tumejifunza utakapotaja mambo kama hayo wale wasiotutakia mema, wanafungua kesi kesho na kesho kutwa watajua mna kiasi gani, maana nyumba yenye mali ndio wezi uinyemelea lakini ndani ya Serikali watajua’ Prof. Kabudi