Leo February 27, 2018 Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho wameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa Kituo Kikuu cha Polisi tangu saa sita mchana.
Viongozi hao waliripoti kituoni leo Jumanne February 27, 2018 na kuachiwa saa 1 usiku, Walienda kituoni hapo baada ya Mbowe kumaliza mkutano wake na waandishi wa habari makao makuu ya chama.
Wakili wa viongozi hao, Frederick Kihwelo ameeleza kuwa wote wameachiwa kwa dhamana kwa kutakiwa kuwa na mdhamini mmoja na kutakiwa kuripoti tena March 5, 2018.
MBOWE NA VIONGOZI WENGINE WA CHADEMA WALIVYOFIKA POLISI KURIPOTI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA