Club ya wekundu wa Msimbazi Simba leo Jumapili ya September 17 2017, baada ya sare tasa dhidi ya Azam FC katika uwanja wa Mbande Chamazi, leo ilikuwa mwenyeji wa Mwadui FC katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam na wamecheza game yao ya tatu ya Ligi Kuu ya Vodacom.
Simba baada ya kumkosa Emmanuel Okwi katika mchezo dhidi ya Azam FC kwa kuchelewa kurudi kutoka Uganda alipokuwa akiitumikia timu yake ya taifa ya Uganda, leo alikuwepo uwanjani na kufanikiwa kufunga magoli mawili katika ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Mwadui FC.
Emmanuel Okwi katika ushindi wa magoli 3-0 wa Simba alifunga magoli mawili dakika ya 7 na 68 na baadae John Raphael Bocco aliyejiunga na Simba msimu huu akitokea Azam FC kufunga goli la mwisho la Simba dakika ya 72 na kuhitimisha idadi ya magoli matatu.
Ushindi huo sasa unaifanya Simba kufikisha jumla ya point saba katika Ligi Kuu msimu huu, ikiwa imecheza michezo mitatu sare moja na ushindi michezo miwili, hivyo wapo nafasi ya pili kwa kuwa na jumla ya magoli 7 Mtibwa ikiongoza kwa point tisa.
Emmanuel Okwi leo baada ya kufunga magoli mawili anakuwa kafunga jumla ya magoli 6 katika Ligi Kuu msimu huu akicheza mechi mbili za Simba, hiyo ni baada ya kufunga magoli manne katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting, Simba ikipata ushindi wa 7-0, Simba hadi sasa haijaruhusu goli.
Video ya dakika 3 ya magoli ya Taifa Stars vs Botswana September 1 2017, Full Time 2-0