Jumamosi ya April 8 2017 uwanja wa Taifa Dar es Salaam timu ya Dar es Salaam Young Africans ilicheza mchezo wake kwanza wa round ya pili hatua ya mtoano kuingia makundi ya Kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya MC Alger.
Yanga walikuwa wanacheza na timu ambayo imewahi kutwaa taji la club Bingwa Afrika mwaka 1976 na imewahi kutwaa Kombe la Ligi Kuu Algeria mara 7, historia na mafanikio ya MC Alger katika soka la Afrika haijainuru na kipigo kutoka Yanga.
MC Alger ambao walionekana kucheza soka la taratibu na kujiami wamejikuta wakifungwa goli 1-0 baada ya wachezaji wa Yanga kupiga pasi nyingi kabla ya Obrey Chirwa kutoa pasi ya mwisho ya goli dakika ya 61 na Thabani Kamusoko akapachika goli la ushindi kwa Yanga.
Kwa matokeo hayo sasa Yanga watakuwa na safari ya kuelekea Algers nchini Algeria kucheza mchezo wao wa marudiano dhidi ya MC Alger lakini ili waweze kutinga hatua ya makundi ya Kombe la shirikisho barani Afrika, watalazimika kupata ushindi au sare yoyote ugenini ili waitoe MC Alger April 15 2017.
FULL HD: AyoTV ilikwenda mpaka Comoro na kunasa magoli yote ya N’gaya vs Yanga, FT: 1-5