Waziri wa Nishati, January Makamba amelielekeza Shirika la Umeme (TANESCO) kuhakikisha kwamba pamoja na kadhia ya umeme inayoendelea, Shirika hilo lisijiingize kwenye kukodi mitambo ya dharura kutokana na historia mbaya ya mitambo ya aina hiyo kuwa na gharama kubwa kwa Serikali na kugubikwa na utata mwingi.
Badala yake Makamba amelielekeza Shirika kuhakikisha kwamba linaongeza miradi mipya ya uzalishaji umeme kwa njia ya upepo na jua ambayo inaweza kutekelezwa ndani ya mwaka mmoja ili mwakani katika kipindi kama hiki cha ukame Taifa lisikabiliwe tena na uhaba wa umeme.
Pia amewaelekeza TANESCO kama Msimamizi wa mradi wa kufua umeme wa Mwalimu Nyerere, Rufiji, ihakikishe kwamba mradi huo hauchelewi kwa kiwango kikubwa ili nao uchangie katika majawabu ya kudumu ya upatikanaji wa umeme nchini.
Waziri Makamba amewasihi Wananchi wawe na subira katika kipindi hiki kigumu wakati TANESCO ikihakikisha kwamba inadhibiti upungufu wa uzalishaji kwa njia mbalimbali ——— “Nimeingia katika nafasi hii katika siku 70 tu zilizopita, wajibu wangu ni kumsadia Rais wetu Mhe Samia Suluhu Hassan, na kuisaidia nchi yetu, kwa kuisimamia TANESCO ipasavyo ili itimize wajibu wake na tuondokane na kadhia hii haraka iwezekanavyo”
BILIONEA LAIZER APATA TENA MADINI YA BILL 3,WAZIRI BITEKO AFIKA