Ni wiki moja tu imepita baada ya kuondoka Mwanza nilikokwenda kwa ajili ya Tour ya Fiesta inayoendelea kwenye mikoa mbalimbali Tanzania ambapo mara zote ambazo nimekua nikiitembelea Mwanza, kila nikitazama watu walivyojenga pembeni au karibu ya mawe makubwa milimani huwa maswali hayaniishi.
Mara zote ninapoitembelea Mwanza Kwenye kumbukumbu zangu sikumbuki kama niliwahi kusikia kuporomoka kwa haya mawe lakini kama Bindamu niliwahi kuwa na hofu hiyo.
Natoa pole sana kwa ndugu waliopoteza ndugu zao wanne baada ya mvua kunyesha kisha nyumba zao kuporomokewa na haya mawe makubwa maeneo ya Mabatini Sinai mtaa wa Nyerere A.
Ni halali yako kupata kila tukio linalonifikia, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB