Familia moja yenye watu zaidi ya 10 wakiwemo watoto wadogo katika mtaa wa Nazareth manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma.
Wamelazimika kuishi nje kwa zaidi ya wiki moja sasa na wanafunzi waliopo kwenye familia hiyo wakisitisha masomo kwa kutokwenda shule baada ya watu wanaodaiwa kuwa askari mgambo pamoja na dalali kuvamia makazi yao na kuwaondoa kwa nguvu kwa madai ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuuzwa baada ya Baba yao kukopa pesa Million 10 na kushidwa kulipa.
Ayo TV na Millardayo.com alimtafuta Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ester Mahawe ili aweze kuzungumza kuhusiana na tukio hilo.
“Nilipata taarifa ya familia hiyo na kwamba familia Iko nje Sasa takribani wiki moja,Ofisi yangu inafatilia hilo kwa ukaribu Sana kuona namna gani kumaliza jambo hili ikiwezekana nje ya mahakama lakini kama hatutaweza kulimaliza nje ya mahakama basi ushauri wa ofisi ya Mkuu wa wilaya itakua nikuhakikisha mlalamikaji au mdaiwa anakata rufaa kabla muda haujaisha lakini kwa Sasa nishauri familia hiyo wasikutwe nje na msimu huu wa mvua ulioko karibu watafute ndugu wakati ofisi yangu inashughulikia mgogoro huu”— Ester Mahawe DC Kigoma
Lakini pia tuliweza kumtafuta Dalali Anayedaiwa Kusimamia zoezi hilo kwa njia ya simu na akaweza kuzungumza kuhusiana na hili na sababu ya kuuzwa hiyo nyumba.
“Hivi mimi ninaweza kukurupuka tu nikaenda kuuza nyumba,hiyo nyumba tumeuza mwaka jana January 15 kwa oder ya mahakama ya Mwanzo anadaiwa milioni 13 na laki Tano,na alikata rufaa akaenda mahakama ya Mwanzo akashidwa,na mchakato uko kihalali”— Job Gwassa Dalali aliyuza Nyumba
BABA AKOPA MILIONI 10 RIBA YAPANDA ASHIDWA KULIPA WATOTO WALIA ”NYUMBA IMEUZWA TUMELALA NJE WIKI”