Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla leo August 18 amepokea Mwenge wa Uhuru uliowasili Asubuhi ya leo Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere ukitokea Mkoa wa Pwani na kuukabidhi kwa Wilaya ya Ilala kwaajili ya kuanza shughuli ya uzinduzi na uwekaji mawe ya msingi kwenye miradi ya miradi ya maendeleo.
Akipokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Aboubakar Kunenge, RC Makalla amesema kwa siku tano ambazo Mwenge wa Uhuru utakuwa Dar es salaam utapitia miradi ya maendeleo 46 yenye thamani ya Shillingi Billion 105.1.
Mwenge wa Uhuru umeanza rasmi kukimbizwa leo Mkoa wa Dar es salaam kwa kuanzia Wilaya ya Ilala Kisha Ubungo, Kinondoni, Kigamboni na Temeke ambapo ifikapo August 23 Mwenge huo utakabidhiwa kwa Mkoa wa Lindi ukienda na kaulimbiu inayolenga kuhimiza Matumizi sahihi ya TEHAMA