Picha 10:Viongozi na Wasanii waliofika kwenye hafla ya Mchongo wa “Big Joe”
Share
2 Min Read
.
SHARE
NI Agosti 6, 2021 ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga aliwaalika watu mbalimbali wakiwemo viongozi na wasanii kushuhudia mchongo wa ‘Big Joe’ utakaosaidia Vijana 55 ili wakajiendeleze katika Biashara zao.
Joseph Kusaga leo ametoa mchongo kwa Vijana 55 wa shilingi Milioni 550 ili tu waweze kukuza biashara zao. Na miongoni mwa watu waliohudhuria hafla hiyo ni Mbunge Mwana FA, DC Godwin Gondwe, Professor Jay, Kelvin Twissa,Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo na wengineo
.Mtangazaji Millard Ayo ni miongoni mwa vijana waliowahi kupita kwenye mchongo wa Big Joe na katika hafla hii kaeleza namna Joseph Kusaga alivyomfungulia Dunia.Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe akizungumza machache katika hafla hiyo.Mtangazaji na Mwimbaji Jose Mara aliwaburudisha na kuwaimbisha katika hafla hiyo..Pichani: Mbunge wa Mtama, Mh Nape Moses Nnauye akitoa burudani katika hafla hiyo.Pichani(Kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga akiwa jukwaani na Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo ambae alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya mchongo wa Big Joe uliofanyika katika ofisi za Clouds Media Group Mikocheni.Pichani(Kushoto) Msanii wa Bongo Fleva,Maua Sama akiwa na Professor Jay katika hafla ya Mchongo wa Big Joe iliyofanyika Clouds Media Group Mikocheni DSM.Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga akiwa na familia yake katika hafla hiyo.Pichani:Vijana 55 waliokula mchongo wa Big Joe wa Milioni 550 ambayo itaenda kukuza biashara zao
MILIONI 550 ZA BIG JOE ZILIVYOKABIDHIWA LEO KWA VIJANA WAFANYABIASHARA