Kutoka Mahakama ya Kisutu leo hizi ni picha za matukio mbalimbali yakiwemo yale ya baadhi ya Wafuasi wa CHADEMA waliofika Mahakama hapa kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, kukamatwa na Askari Polisi baada ya kuinua mabango na kupiga kelele kwamba “Mbowe sio Gaidi”.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekwama kuendelea kusikiliza kesi hiyo ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kutokana na hitilafu ya mtandao.
Kesi hiyo inayosikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ilipangwa kuendeshwa kwa njia ya mtandao “Video Conference” lakini imeshindikana kutokana na tatizo la kimtandao, Wakili wa Mbowe, Peter Kibatala amesema kutokana na sababu hizo, Mbowe atafikishwa Mahakamani kesho August 6, 2021 badala ya kesi hiyo kuendeshwa kwa njia ya mtandao.
Mbowe alifikishwa Mahakamani hapo kwa mara ya kwanza July 26, 2021 kwa mashtaka mawili ikiwemo la tuhuma za Ugaidi.
MTANDAO WAKWAMISHA KESI YA MBOWE, MAHAKAMA YATOA MAELEKEZO “WALIOKAMATWA TUNAWAFATILIA”