Kampuni ya mafuta ya Total imetangaza mabadiliko kwenye jina lake na sasa inakuwa TotalEnergies ambapo uzinduzi wa jina na nembo mpya na kituo chake cha kwanza cha huduma ya umeme wa jua umefanyika leo Samora Avenue Dar es salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Nishati January Makamba, Balozi wa Ufaransa Tanzania Nabil Hajlaoui, Mwenyekiti Mtendaji VP Olagoke Aloui na wengine.
Pamoja na hotuba yake ya mabadiliko haya ya safari mpya ya mabadiliko ya nishati Mkurugenzi wa Mtandao wa Biashara wa TotalEnergies Marieme Sow pia aliwashukuru Wateja wote Nchini kwa imani yao na kuifanya TotalEnergies kuwa kampuni namba 1 ya mafuta Tanzania.
Aidha Makamba ameeleza sababu ya kupanda kwa bei ya Mafuta na kusema…”Kupanda kwa bei ya mafuta nchini imesababishwa na kile kinachoendelea katika vita ya Urusi na Ukraine, Serikali ipo katika majadiliano kutatua hilo kwahiyo tuwaondoe hofu Wananchi na wala sio kama tumelikalia kimya:- Waziri Makamba
Hizi ni baadhi ya picha kutoka katika uzinduzi huo wa kituo cha Mafuta.
.
AJALI YA BASI NA LORI IDADI YA VIFO YAFIKIA 23, MAJERUHI WAFUNGUKA “NILIPOTEZA FAHAMU”