Jumla ya watoto sita waliozaliwa wakiwa na vichwa vikubwa mkoani Tabora wamefanyiwa upasuaji huku wengine 30 wakipata maelekezo ya jinsi ya kukabiliana na hali hiyo bila ya kuwa mzigo kwa jamii iliyowazunguka katika awamu ya nne ya kambi tiba za GSM Foundation zinazoendeshwa kwa kushirikiana na madaktari Bingwa kutoka Taasisi ya Upasuaji na Mifupa ya Muhimbili MOI.
Idadi hii inasababisha jumla ya watoto waliotibiwa na kambi tiba hizo zilizoanza mwezi Aprili mwaka huu na kupita zaidi ya mikoa 15 kufikia watoto 196 huku kambi ikiwa bado inaelekea kuifikia mikoa mitatu zaidi ya Tanzania Bara na baad ya halo kuelekea Visiwani Zanzibar mapema mwezi Novemba mwaka huu.
Akiongea na wanahabari kabla ya kufunga kambi tiba hiyo inayotembea na madaktari Bingwa wanne, amnesie wanne na mabwana usingizi wawili, Kaimu Mkuu wa kambi tiba hiyo Dk Hamis Shaaban amesema bado kuna changamoto ya uelewa kwa wazazi wenye watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa ambapo wengi wao bado hawaamini kwamba tiba za kitabibu zinaweza kumaliza tatizo la watoto wao.
“Wengi wao bado wanaamini kwamba tatizo hili ni la kulogwa hivyo huwaficha watoto wao kwa waganga wa kienyeji, na mpaka tunapowafikia tunakuta muda wa kuweza kuokoa afya na maisha yao kwa ujumla unakuwa umeshapita”, >>> Shaaban.
Kwa upande wake Afisa Habari wa GSM Foundation, Khalphan Kiwamba amewaomba wananchi walioa mikoa ya Kagera, Kigoma, Rukwa na Zanzibar ambako kambi tiba hiyo inaelekea kujitokeza ili kuipata fursa hiyo ambayo hakuna hakika kwamba inaweza kutokea tena katika miaka ya karibuni.
“Gharama ya kumtibu mtoto mmoja mwenye kichwa kikubwa ni karibia shilingi milioni moja za kitanzania, lacinié GSM Foundation imelipia gharama zote za tiba kwh mikoa yote ya Tanzania kea mwaka huu na huenda mwakani tussle na kambi za namna hii. Kwa hiyo tujitahidi kuchangamkia fursa”>>> Kiwamba.
ULIMISS UCHAMBUZI WA MAGAZETI YA LEO OCTOBER 20? NIMESHAYAWEKA HAPA