Baada ya hivi karibuni Mkurugenzi wa Kampuni ya Uzalishaji na uuzaji wa Maziwa ‘Asas’, Ahmed Asas kufunguka kuhusu kuelekea kwa kampeni ya uhamasishaji kuhusu juu ya utoaji wa Elimu visiwani Zanzibar.
Sasa leo miongoni mwa waliopata nafasi ya kutembelewa ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman ambae kwenye mazungumzo alisema anaitambua kampeni ya uhamasishaji ya maziwa inayoendelea visiwani Zanzibar ambayo itafikia kilele chake Juni 17, mwaka huu katika Viwanja vya Kisonge na kuwataka wananchi kufika kujua Elimu itakayotolewa kuhusu Maziwa.
‘Tunawashukuru Asas ujio wenu wa hiyo kampeni ya ‘Jali Afya na Asas’ na pia ni wakati sasa kweli kwani Sekta ya Mahoteli hapa Zanzibar imekua kwa kasi ni zaidi ya hoteli mia 600 zinatoa huduma kwa watalii hivyo ndio wakati wenu muende mkatoe Elimu juu ya unywaji wa Maziwa, Maziwa ni Afya kwa kila Wananchi’- Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman
‘Mwisho ningependa sasa kuwaomba Wananchi wote wafika katika kilele chake June 17, 2023 pale kwenye viwanja vya Kisonge ili Elimu hii aipate kila Mwananchi ni bure wala haina gharama yoyote Jali Afya yako wewe Mwananchi na Asas’-Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman