Baada ya hivi karibuni Mkurugenzi wa Kampuni ya Uzalishaji na uuzaji wa Maziwa ‘Asas’, Ahmed Asas kufunguka kuhusu kuelekea kwa kampeni ya uhamasishaji kuhusu juu ya utoaji wa Elimu visiwani Zanzibar.
Sasa leo miongoni mwa waliopata nafasi ya kutembelewa na Asas ni Waziri wa Afya, Mh Nassor mazrui ambae kwenye mazungumzo alisema anaitambua kampeni ya uhamasishaji ya maziwa inayoendelea visiwani Zanzibar ambayo itafikia kilele chake Juni 17, mwaka huu katika Viwanja vya Kisonge na kuwataka wananchi kufika kujua Elimu itakayotolewa kuhusu Maziwa.
‘Kwanza kabisa ningependa kuwashukuru Asas kwa kuja ofisni kwangu kingine kilele cha kampeni hii ya Jali Afya na Asas ni June 17, 2023 pale Viwanja Vya Kisonge wewe Mwananchi fika kutakuwa na mambo mengi kwani unywaji wa Maziwa ni Afya kwa wewe Mzanzibar mnakaribishwa wote’