Mapema ya Jana Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa kutokea Mkoa wa Mtwara Cde. Sameer Hasnain Murji alifanya ziara ya kikazi Kwa mujibu wa Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Wilayani Masasi na kufanya shughuli mbali mbali za kuimarisha chama ambapo pamoja na mambo mengine.
Mbaraza SAMEER MURJI amegawa Jezi na mipira Kwa Timu mbili za kata ya Lukuledi na Timu mbili za kata ya Napupa pia amekabidhi Mchele,Unga na nyembe Kwa shule Maalum ya kata ya Lukuledi na amewakabidhi kikundi Cha Vijana wanaochimba madini ya changa chepe(spade) 5 kuunga juhudi kazi wanazo zifanya vijana hao.
Mbaraza Sameer Murji ameeleza kuwa Mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Ibara ya 18 Kipengele kidogo Cha Kwanza kinasema mtu yeyote Mwenye Umri Kuanzia Miaka 18 Nakuendelea anayohaki yakugombea nafasi katika Uchaguzi Wa Serikali Za Mitaa pamoja na Uchaguzi Mkuu, Udiwani,Ubunge.
Mbaraza Sameer Murji pia Ni Mjumbe wa Halmshauri kuu CCM Mkoa Wa Mwara amewatoa hofu Vijana kuachana kuogopa vitisho Vya Watu au Makundi ya Watu Wenye Ubinafsi na Wenye Uroho wa Madaraka ya Uongozi,amehaidi kuwapmbania Vijana kwakusimamia katika Vikao ili Majina Yao Yaweze kurudi.
Mbaraza ameongea maneno hayo Mbele ya Vijana Wilayani Masasi kutokana na Kasumba za Baadhi ya Viongozi Wanajifanya Miungu watu kutohitaji Vijana Kuchukua form za kugombea Uchaguzi, hitaji Lao kuona kila siku Vijana Wawe Wabeba Mizigo,Mabango na kuwasifia Wao.
MBARAZA CDE Sameer Murji amewataka Vijana kutenga muda wa kusoma historia ya Nchi Kuweza kufahamu Maendeleo yaliyoletwa kutokana Uzalendo, na Ujasiri na Ukokomavu katika Harakati za Kupigania Uhuru Wa Taifa letu wakiwa katika Umri Wa Miaka 29-30 wakafanikiwa Kupata Uhuru wa Taifa letu.
Mbaraza aliwaimiza Vijana kuyaishi Maono ya Muasisi wetu Baba Wa Taifa Mwalimu Nyerere namna alianza Uongozi wake alisema, Baada ya Kupata Uhuru Baba Wa Taifa aliendeleza kuwaamini Vijana Kuwa ndio wenye nguvu Katika kukuza Shughuli za kiuchumi Pia aliweza kutoa mifano ya Miongoni Mwa Vijana walioweza kuaminiwa akiwa na umri mdogo wakati Wa Uongozi wa Mwalimu Nyerere DKT SALIM HAMDI SALIM kuwa Katibu Mkuu Wa Umoja wa Mataifa pia Alifanya vizuri akawa Balozi Nchini MiSri.
Aidha Mbaraza CDE Sameer Murji amegusia kuhusu fursa Kwa vijana na kuwataka Vijana kufanya bidii katika kukimbilia fursa zitakazo jitokeza Kwenye Maeneo yao na kutosita kuchukua Mikopo inayo tolewa na Halmashauri zetu pindi asilimia 10 itakapo rejea Tena .
Mwisho Mbaraza amepongeza Uongozi wa Jumuiya ya Umoja wa vijana Wilaya ya Masasi kwakuweza kushirikiana pamoja na Vijana wa Bodaboda kwa Mapokezi makubwa na Mwisho Mjumbe wa baraza kuu Taifa ameomba kwa Wana CCM 2025 form ya kuomba Urais ni moja tu ya Samia Suluhu Hassan na tuendelee Kumuunga Mkono katika jitihada anazo tufanyia MAMA yetu Dkt Samia Suluhu Hassan.