Ni June 28, 2023 ambapo Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Jokate Mwegelo ametembelewa na Mke wa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mama Fatma Karume Wilaya humo Mkoani Tanga.
Akizungumza na Millardayo.com DC Jokate Mwegelo alisema..’Imekuwa faraja sana leo na heshima kubwa sana kwangu kutembelewa Wilayani Korogwe na Mke wa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mama Fatma Karume. Alifika ofisini na tukapata wasaa wa kula pamoja na kuongea nje ya ofisi‘-Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Jokate Mwegelo
‘Mama Fatma Karume ni kielelezo halisi Cha katika kila mafanikio ya mwanaume kuna mwanamke nyuma yake kwani ni dhahiri shahiri alikuwa na wajibu mkubwa sana kwenye mafanikio ya mumewe Sheikh Abeid Amani Karume kabla na baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyowapa haki na uhuru wa kujitawala na kujiamulia mambo yao Wananchi wa visiwa vya Zanzibar’- Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Jokate Mwegelo
‘Kwa muda mfupi amenipa hamasa na ujasiri katika kutekeleza majukumu ya umma nikiwa kama Mama wa familia na kiongozi. Ila zaidi nimependa ni mcheshi sana, mama mwenye upendo na amebeba hadithi nyingi nzuri zenye kubeba historia njema ya nchi yetu’- Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Jokate Mwegelo
‘Katika mengi tuliyoongelea tuligusia pia kidogo timu ya wananchi @yangasc nikamweleza napenda kuona Wanawake wengi zaidi kama yeye kwenye uongozi pale juu, Nakuombea afya njema na umri mrefu zaidi Inshaallah Karibu tena Ko’ogwe ni nyumbani kwako’- Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Jokate Mwegelo