Ni February 28, 2024 ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Dkt. Bill Kiwia amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA) Juma Burhan Mohamed katika ofisi za HESLB jijini Dar es salaam na kukubaliana kuanzisha ushirikiano ili kuongeza kasi ya urejeshaji wa mikopo kutoka kwa wajasiriliamali walionufaika na mikopo ya elimu ya juu.
Kikao hicho pia kilikubaliana kuendelea kutafuta fursa za ajira kwa wahitimu walionufaika na mikopo ya elimu ya juu ili kuwawezesha kurejesha.
ZEEA ilianzishwa mwaka 2022 ikiwa na lengo la kuimarisha mazingira kuwawezesha wananchi kiuchumi ili kuongeza uzalishaji na masoko ya bidhaa za wajasiriliamali.