Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Kampasi ya Mwanza kitivo cha Mawasiliano ya Umma (PR) kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWT) kikosi cha Mwanza Transit Camp (MCT) pamoja na Synergistic Globe wamepanda miti 500 katika eneo la wazi lengo likiwa ni kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Shughuli hiyo ya upandaji miti imeambatana na mbio fupi za kuhamasisha utunzaji wa mazingira zikiwa na kauli mbiu ‘Miti kabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupanda miti milioni 1.5 kwa kila halmashhauri nchini.
Kiongozi wa tamasha hilo Mhadhiri wa kitivo hicho Tabu Manyama amesema suala la utunzaji wa mazingira ni jukumu la kila Mtanzania hivyo ni vizuri Wanafunzi kufanya shughuli za namna hiyo ili wawe Mabalozi katika jamii zao.
JESHI LA WANANCHI Vs CHUO CHA SAUT WAUNGANA KUKABILIANA MABADILIKO YA TABIA NCHI