Young Africans SC kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar leo imewaalika Klabu ya Kaizer Chiefs kutembelea Visiwa vya Zanzibar kama sehemu ya utalii katika visiwa vyenye vivutio bora.
Msafara huo ambao unaongozwa na Rais wa Young Africans Eng.Hersi kwa uenyeji wa Makamu wa Rais Arafat Haji wakiwa na Wageni wao chini ya BOBBY KAIZER utatembelea maeneo kadhaa ya vivutio na historia ya visiwani Zanzibar.