Kamanda wa Kanda maalum Da es Salaam Jumanne Muliro Jumanne amekabidhi magari matatu ya Usalama barabarani aina ya Pro box yaliyonunuliwa na kamati ya Usalama barabarani Mkoa wa Temeke kwa thamani ya jumla ya milioni 48.
Huku kila gari moja likigharimu milioni 16 ambapo Kampuni ASAS ikiwakilishwa na Faraji Abdi ikichangia zaidi ya milioni 9 kuboreshwa kwa magari hayo.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika hafla hiyo Jijini Dar es Salaam Kamanda Muliro amewaonya askari watakao tumia vibaya magari hayo kuadhibiwa.
“Uzito wa makosa ya tuhuma tutakazozipata utakazokuwa ukizifanya wewe askari Polisi huku ukilitumia gari hili la Polisi ambao kamati ya usalama barabarani ya Mkoa wa Temeke imeamua kuyanunu alafu wewe ukaenda kufanyia vitu vya ovyo maamuzi ya kitendo ulichokifanya yatalingana na uzito wa udhalilishaji ulioufanya kwenye jeshi la polisi lakini pia kwenye udhalilishaji wa usalama barabarani”-Kamanda Muliro