Kamati ya kudhibiti UKIMWI ya Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam (CMAC) imefanya ziara ya kutembelea na kufuatilia maendeleo ya kikundi cha Upendo kwa Wote kilichopo Chanika ambacho ni kati ya vikundi wezeshi vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la watu wanaoishi na VVU ( NACOPHA). NACOPHA wanatekeleza mradi wa Hebu Tuyajenge unaofadhiliwa na serikali ya watu wa marekani (PEPFAR/USAID).
Katika ziara hiyo, kamati imepata nafasi ya kushuhudia shuguli za kikundi hicho ambazo ni ufugaji wa ng’ombe, kilimo cha Mahindi, mapapai, ndizi na mboga mboga pamoja na ukaushaji wa matunda.
Kamati imefurahishwa sana na maendeleo makubwa ya kikundi ambayo yamechangiwa na usaidizi wa kiuchumi kupitia mikopo ya Halamshautu ya 4-4-2.
Aidha Kiongozi wa msafara Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo Bi Lucy Lugome amehaidi kuendelea kuunga mkono juhudi za kikundi cha upendo kwa wote.. “Tunaahidi kufanya mapitio yalioombwa kupitia taarifa iliyosomwa ili kuwezesha kikundi hiki kupata usaidizi zaidi ili kufikia malengo yenu na tutaendelea kutoa ushirikiano unaohitajika ili kuhakikisha kuwa mnapata maendeleo endelevu”
Ziara hii imehusisha wataalamu ambao ni mwanasheria wa jiji, Mchumi na afisa maendeleo ambao kwa pamoja waliombwa kuangalia namna ya kuinua kikundi cha Upendo kwa Wote na pia kutumia kikundi hiki kama mfano kwa ajili ya kutoa usaidizi kwenye vikundi vingine.