Kamati ya kudumu ya Bunge ya uwekezaji wa mitaji ya umma imetembelea na kuridhishwa na mwendelezo wa kiwanda cha sukari Cha mkulazi na kuona maendeleo yake ambapo Kamati hiyo imeridhishwa kwani kiwanda hiko kimekamilika kwa Asilimia 98.
Akizungumza na Waandishi wa habari Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya uwekezaji wa mitaji na umma Vuma Augustin amesema Kiwanda hiki kitaenda kumaliza changamoto ya sukari ambayo imekuwa kilio kikubwa kwa watanzania.
Hata hivyo Hildelta Msita Mwenyekiti bodi ya Mkulazi amesema mpaka sasa Kiwanda Cha mkulazi tayari kimeanza uzalishaji na sukari tayali ipo sokoni na wameipongeza kamati ya Kudumu ya Bunge kwa kufika na kutembelea hali ya maendeleo ya Kiwanda hiki.
Kwa Upande wake mjumbe wa Bodi ya wadhamini NSSF Lucy William naye amesema ameridhishwa na ujio wa kamati hii pia Baadhi ya maagizo yalitolewa na kamati watayafanyia kazi ili kufanya Kiwanda kufanya kikamilike kwa asilimia 100 ili kumaliza kabisa changamoto ya sukari.