Ni February 28, 2024 ambapo Makamu Mwenyekiti UVCCM Taifa Ndg. Rehema Sombi Omary (MNEC) ameongoza wajumbe wa kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa kufanya Ukaguzi wa Ujenzi wa majengo mapya katika Hospitali ya Wilaya ya Muheza( Samia Suluhu Hospital), kwa kukagua majengo 14 ambayo ni Jengo la Wazazi, jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD), stoo ya dawa, Mionzi, Maabara, Utawala, Kuhifadhia maiti, upasuaji, Wodi ya watoto, Wodi ya upasuaji wanawake, Wodi ya Upasuaji wanaume, Wodi ya wanawake magonjwa mchanganyiko, Wodi ya waname magonjwa changanyiko na nyumba ya mtumishi (three in one), Iliyogharimu kiasi cha Tsh Tshs 3,718,529,827 kutoka Serikali Kuu.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Muheza Mh.Hamis Mwinjuma na N/Waziri wa Sanaa, Michezo na Utamaduni ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Awamu ya Dkt Samia Suluhu Hassan kwa mabilioni ya ujenzi huo. Nae ametoa Vitanda 24 vya wagonjwa katika hospitali.