Ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Daniel Chongolo katika ziara yake Mkoani Mtwara amewahakikishia wananchi wa Mtwara kuwa usafirishaji wa zao la Korosho kuanzia mwaka huu utafanyika katika bandari ya Mtwara na kuwahakikishia kuwa Serikali inalitilia mkazo suala hilo.
Cde. Chongolo amesema kuwa kutumika kwa bandari ya Mtwara ni moja kati ya mkakati wa utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kwani Serikali ipo katika mchakato wa kufanya maboresho makubwa katika sekta ya usafirishaji wa majini.