Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (The U.S. Center for Disease Control -CDC) kupitia Shirika la Amref Health Africa Tanzania kwa ufadhili wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) kimetoa msaada wa vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) katika mkoa wa Mara na Simiyu kwa ajili ya utunzaji sahihi wa takwimu kwa kuondoa makosa na urudiaji wa usajili wa mteja pamoja na kutatua changamoto ya utambuzi wa kawaida wa wateja wapya na wa zamani wanaopata huduma katika vituo vya tiba na matunzo.
Mratibu wa PEPFAR Tanzania Jessica Greene pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Kituo cha Kudhibiti Magonjwa nchini Marekani (CDC) Tanzania Dkt. Mahesh Swaminathan wameshuhudia makabidhiano hayo katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.
Akizungumza Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania Dkt. Florence Temu ameeleza kuwa vifaa hivyo vimenunuliwa kupitia Mradi wa Afya Kamilifu unaotekelezwa na Amref Health Africa Tanzania kwa ufadhili wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI – The U.S. President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR) kupitia Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (The U.S. Center for Disease Control -CDC).
“Kupitia muongozo wa Wizara ya Afya (NACP), Amref Tanzania imenunua vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) 155 vyenye thamani ya Tsh. 25.”
Dkt. Florence Temu ameongeza wametoa mafunzo kwa vitendo kwa viongozi wa Afya wa mkoa na wilaya na wahudumu wa Afya kwa halmashauri zote juu ya matumizi ya utambuzi wa vidole kupitia jmfadhili PEPFAR.