Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Philip Mpango amezindua Kituo Kikuu cha Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Dar es salaam kilichopo Wilaya ya Temeke.
Katika uzinduzi huo, Makamu wa Rais Dr. Mpango amesisitiza kwa Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wote kuilinda na kutunza miundombinu kwani hiyo ni faida kubwa na hasa kwa miundombinu ya Zimamoto na Uokoaji.
Hata hivyo Makamu wa Rais, Dr. Mpango pia ameshuhudia onyesho la Askari wa Zimamoto na Uokoaji la namna ya kufanya uokozi katika majengo marefu wakati alipowasili katika hafla ya Uzinduzi wa Kituo Kikuu cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dar es salaam kilichopo Wilaya ya Temeke.